Mhe. Balozi Philip S. Marmo wa Ubalozi wa Tanzania Ujerumani yuko Vienna, Austria tarehe 9 Septemba, 2014 kuweka saini Mkopo kwa mradi wa tatu wa kupunguza umasikini wa Dola za Marekani 16,350,000 na mradi wa kuendeleza Elimu wa Dola za Marekani 10,200.000. Miradi hiyo itatekelezwa na serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Mheshimiwa Balozi Marmo anawakilisha pia Austria kutoka Ujerumani. Mkataba huo ulisainiwa katika ofisi za OFID, Vienna, Austria kati yake na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa OPEC kwa ajili ya Maendeleo ya Kimataifa, OPEC Fund for International Development(OFID) Bw. Suleiman J. Al-Herbish.
Balozi Philip S. Marmo akiweka saini Mkataba wa Mkopo kutoka Mfuko wa OPEC , OFID Ofisi ya OFID iliyopo Austria, Vienna tarehe 9 Septemba, 2014.
Balozi Marmo akipokea Nakala ya Mkataba wa Mkopo kutoka Mfuko wa OPEC kutoka kwa Bw. Suleiman J. Al-Herbish, Mkurugenzi Mkuu wa OFID-Mfuko wa Maendeleo wa OPEC , Austria, Vienna tarehe 9 Septemba.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Hata mkopo wa Zanzibar lazima kiongozi wa Tanganyika arizie? Haya ndio yanayo tukera. Bila ya heshima bora twende kwenye hizo 3 ama tubaki na 2 kila upande na yake.

    ReplyDelete
  2. Unalalamika mkopo kuriziwa na balozi wa Tanzania mbona huwa hamkerwi na mishahara ya wafanyakazi wa Serikali kutoka hazina bara? Acha siasa nyepesi x2

    ReplyDelete
  3. Huyo si balozi wa Tanzania....moja ya kazi zake ni kusimamia shughuli zote za nchi kwenye nchi za nje. Sasa tatizo lipo wapi akisimamia mikopo yote ya jamhuri ya muungano? Serikali kuu ndiyo msimamizi wa mikopo kwa serikali ya ZNZ na ya muungano. Kama mnaendelea kulalamika mkajilipie wenyewe na muwe wadhamini kwa mikopo yenu huko ZNZ kwa kuwa hamlaimishwi kusimamiwa na balozi zetu. Kila kitu malalamiko pamoja na kupewa pesa za bure.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...