THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.


Share Michuzi Blog

NHIF WAZINDUA MPANGO WA HUDUMA ZA MADAKTARI BINGWA MANYARA.

 Meneja wa NHIF Mkoa wa Manyara, Innocent Mauki akiwakaribisha viongozi wa NHIF makao makuu na uongozi wa Mkoa wa Manyara, kwenye uzinduzi wa mpango wa huduma za madaktari bingwa Mkoani Manyara. 

Baadhi ya wakazi wa Wilaya ya Babati Mkoani Manyara, wakishuhudia Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dk Joel Nkaya akizindua mpango wa huduma za madaktari bingwa mkoani humo, zilizowezeshwa na NHIF
 Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dk Joel Nkaya Bendera akizungumza asubhi ya leo kwa kuwa mkoa huo kujiunga na mfuko wa afya ya jamii (CHF) kwenye uzinduzi wa mpango wa huduma za madaktari bingwa mkoani Manyara uliowezeshwa na NHIF.
 Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Manyara, Dk Joel Nkaya Bendera (kushoto) akimkabidhi Mganga Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dk Ally Uredi vifaa tiba na dawa zilizotolewa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, (NHIF) ambazo gharama zake ni shilingi milioni 5.5.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA


DR. MENGI AZINDUA MPANGO WA AIRTEL FURSA 'TUNAKUWEZESHA' JIJINI DAR.

  Mwenyekiti Mtendaji wa makampuni ya IPP Ltd, Dk. Reginald Mengi (wa pilikulia), Mwenyekiti wa Bodi ya Airtel Tanzania, Balozi Juma Mwapachu (wapili kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Sunil Colaso (kulia) na Menejawa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi wakiwa wameshika bango kamaishara ya uzinduzi wa mpango wa Airtel Fursa ‘Tunakuwezesha’, katika haflailiyofanyika jijini Dar es Salaam  jana.
  Mwenyekiti Mtendaji wa makampuni ya IPP Ltd, Dk. Reginald Mengi (wa pili kulia), akikabidhi zawadi ya pasi na meza yake kwa muuza mitumba RashidSeleman (wa pili kushoto), ambaye ni mmoja wa vijana waliowezeshwa na  mpango wa Airtel Fursa ‘Tunakuwezesha’ katika hafla ya uzinduzi wa mpango  huo, iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji    wa Airtel Sunil Colaso, Mwenyekiti wa Bodi ya Airtel Tanzania, Balozi Juma  Mwapachu (wa tatu kushoto) na Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi.
 Mwenyekiti Mtendaji wa makampuni ya IPP Ltd, Dk. Reginald Mengi (wa pili kulia), akikabidhi zawadi ya mashine ya kutengeneza juisi kwa Abdulkarim  Ramadhan (wa tatu kushoto), ambaye ni mmoja wa vijana waliowezeshwa na mpango wa Airtel Fursa ‘Tunakuwezesha’ katika hafla ya uzinduzi wa mpango huo, iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kutoka (kushoto) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Sunil Colaso, Mwenyekiti wa Bodi ya Airtel Tanzania, Balozi Juma Mwapachu na Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
 


RAIS KIKWETE AWAAPISHA KATIBU MKUU, NAIBU KATIBU MKUU WA MAMBO YA NJE NA BALOZI WA TANZANIA SAUDIA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akimwapisha  Balozi Liberata Mulamula kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Balozi Mulamula anakuwa Katibu Mkuu wa kwanza mwanamke kuongoza Wizara hiyo na kabla ya uteuzi huo alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Marekani. Hafla hiyo fupi ya uapisho imefanyika Ikulu tarehe 27 Mei, 2015.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akimwapisha Balozi Hassan Simba Yahya  kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Kabla ya uteuzi huo Balozi Yahya alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Hafla hiyo fupi ya uapisho imefanyika Ikulu tarehe 27 Mei, 2015.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akimwapisha, Mhe. Hemed Iddi Mgaza kuwa Balozi  wa Tanzania nchini Saudi Arabia. Kabla ya uteuzi huo Balozi Mgaza alikuwa Afisa Mambo ya Nje Mkuu  na Mkuu wa Utawala katika Ubalozi wa Tanzania, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC). Hafla hiyo fupi ya uapisho imefanyika Ikulu tarehe 27 Mei, 2015.
PICHA ZAIDI INGIA HAPAMAADHIMISHO YA WIKI YA UKOMBOZI BARA LA AFRIKA,WANAWAKE WAELEZA NAMNA WALIVYOSHIRIKI KATIKA UKUMBOZI

 Mwenyekiti wa Bodi ya AICC na Mgeni Rasmi wa Maadhimisho ya wiki ya Ukombozi wa Bara la Afrika, Balozi Christopher Liundi akikata utepe katika maadhimisho hayo ikiwa leo ni siku ya Kuona Mchango wa Wanawake katika Ukombozi wa Bara la Afrika, maadhimisho hayo yamefanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam.
Profesa Ruth Meene akizungumza na baadhi ya wanafunzi na watu wengine waliohudhuria (hawapo pichani) ili kujua mchango wa wanawake katika ukombozi wa Bara la Afrika, wanawake hao ambao wamesaidia zaidi ni Mke wa Rais wa Mozambiq,Jocina Machel,Bi Ndaitwa wa Namibia,Winnie Mandela wa Afrika Kusini,Albetina Kisulu,Elizabeth Sebeko,Mariam Makeba wote wa Afrika kusini  na hapa nchini ni Bibi Titi Mohamed,Lucy Maulid na Sophia Kawawa ambao walikuwa wakihamasisha wananchi Kisiasa katika kulikomboa Bara la Afrika.
 Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Victoria waliohudhuria katika Mkutano wa kujua jinsi wanawake walivyoshiriki katika kulikomboa Bara la Afrika, katika Mkutano uliofanyika Makumbusho ya Taifa jijiji Dar es Salaam leo.
 Mwenyekiti wa Bodi ya AICC na Mgeni Rasmi wa Maadhimisho ya wiki ya Ukombozi wa Bara la Afrika, Balozi Christopher Liundi akizungumza leo na waandishi wa habari mara baada ya kutoka katika kumbi zenye  picha na vitu mbalimbali ndani ya jengo la Makumbusho ya Taifa vinavyoonyesha kumbukumbu ya matukio mbalimbali yalivyowahi kutokea hapa nchini.Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.


JK ATOA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA ZA MZEE RUANGISATHE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
Website : www.ikulu.go.tz              

Fax: 255-22-2113425PRESIDENT’S OFFICE,
      STATE HOUSE,
              1 BARACK OBAMA ROAD,  
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amepokea kwa masikitiko na huzuni nyingi taarifa ya kifo cha mwanasiasa mkongwe nchini na aliyepigania uhuru wa Tanganyika, Ndugu Samwel Ntambala Ruangisa, ambaye aliaga dunia mwanzoni mwa wiki hii nchini Marekani ambako alikuwa anatibiwa.

Katika salamu za rambirambi ambazo amempelekea Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Mheshimiwa John Mongella kuomboleza kifo cha Mzee Ruangisa, ambaye pia alikuwa bado diwani katika Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba, Rais Kikwete amesema:

“Nimepokea taarifa za kifo cha Mzee Ruangisa kwa masikitiko na huzuni nyingi. Kwa zaidi ya nusu karne, Mzee Ruangisa amekuwa kiongozi wa kuigwa mfano katika nafasi zote ambazo zimepata kuzishikilia katika maisha yake kuanzia Ukuu wa Mkoa wa Ziwa Magharibi (sasa Kagera) na baadaye Mkoa wa Mara tu baada ya Uhuru wa Tanganyika mwaka 1961, Ubalozi, Uwaziri, Ubunge, Umeya na Udiwani. Katika kila nafasi aliyoishikilia, Mzee Ruangisa alionyesha uongozi wa kiwango cha juu. Kwa hakika, tumepoteza kisima cha uzoefu wa uongozi.”

Rais Kikwete ameongeza katika salamu zake za rambirambi: “Mkuu wa Mkoa nakutumia salamu zangu za rambirambi kuomboleza msiba huu na kupitia kwako naomba uwape pole wana-Kagera wote kwa kuondokewa na mzee wao wa siku nyingi. 

Aidha, naomba unifikishe pole zangu nyingi kwa wanafamilia wote ambao wamepoteza baba, babu na mhimili wa familia. Wajulishe kuwa niko nao katika kipindi hiki kigumu. Waambie naelewa machungu yao kwa sababu machungu yao ni machungu yangu. Vile vile, naungana nao katika kumwomba Mwenyeji Mungu, Mwingi wa Rehema, aiweke peponi roho ya Marehemu Samwel Ntambala Ruangisa. Amina.”

Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
IKULU,
DAR ES SALAAM.

27 Mei, 2015


Tangazo la Kozi ya Masters


Rais Kikwete afungua Mkutano Mkuu wa Chama Cha Waalimu Tanzania (CWT)

 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba yake ya ufunguzi wa Mkutano mkuu wa Chama Cha Waalimu TANZANIA( CWT) uliofanyika katika hoteli ya Ngurdoto nje kidogo ya mji wa Arusha jana.Wakati wa mkutano huo wanachama wa CWT ulitarajia kuwachagua viongozi wapya wa chama Hicho.Akizungumza katika  mkutano huo Rais Kikwete ameahidi kutatua changamoto moto mbalimbali zinazowakabili waalimu nchini(picha na Freddy Maro).


MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AAGANA NA BALOZI WA TANZANIA NCHINI KENYA, JOHN HAULE

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi mpya wa Tanzania nchini Kenya, John Michael Haule, wakati Balozi huyo alipofika Osifini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kumuaga leo Mei 27 2015. Picha na OMR


CHADEMA YAENDELEA KUHAMASISHA WANANCHI KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA JIJINI MWANZA


 Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasi na Maendeleo (CHADEMA) Zanzibar Salum Mwalim akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika hivi karibuni mjini Magu, mkoani Mwanza, ikiwa ni sehemu ya mfululizo wa mikutano ya chama kuhamasisha wananchi kujiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na kujiandaa kupiga kura uchaguzi mkuu Oktoba mwaka huu.
Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lisu akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika hivi karibuni katika Uwanja wa Halmashauri, mjini Bariadi, mkoani Simiyu hivi karibuni alipokuwa mkoani humo kwa ajili yakuzindua mpango maalum uitwao 'Changia Chadema Kanda ya Serengeti ili Kushinda Uchaguzi 2015' unaolenga kukusanya fedha kampeni za wagombea wa ubunge na udiwani mikoa ya Simiyu, Shinyanga na Mara.


Mama wa Mitindo Asia Idarous Khamisin afiwa na Mama yake mkubwa Zanzibar


IMG_3895

MBUNIFU mkongwe wa mavazi, Mama wa mitindo nchini, Asia Idarous Khamsin amepata pigo kufuatia kufiwa na Mama yake mkubwa, Aliyefahamika kwa jina la Fatma Juma, Msiba uliotokea Kisiwa Ndui, Unguja.

Kwa mujibu wa taarifa za msiba huo ambao hata hivyo tayari mazishi yake yamefanyika siku ya Jumatatu ya Mei 25, Kisiwa Ndui, na leo Jumatano ya Mei 27 wanatarajia kufanya kisomo maalum.

Ratiba ya Kisomo:
Leo Jumatano ya Mei 27, saa 10, Alasiri wanatarajia kufanya kisomo maalum kwa wanawake wote nyumbani kwa marehemu, Kisiwa Ndui na kwa upande wa Wanaume wao wanatarajia kufanya kisomo, majira ya saa mbili usiku.

Tunampa pole Mamaa wa Mitindo Asia Idarous Khamsin kwa kufiwa na Mama yake mkubwa na mlezi. 

"Inna lillahi wa inna ilayhi rajiiun, mwenyezi mungu amlaze pema peponi".


KEY LIVE SPORTING EVENTS ON DStv and GOtv 28 May – 07 Jun.Wananchi watakiwa kutoa taarifa za ukiukaji wa kanuni na sheria za usalama barabarani

 Naibu kamishna wa jeshi la polisi kikosi cha Usalama Barabarani SACP Johanes Kahatano(katikati)akiwafafanulia jambo Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia(kushoto) Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Kamishna Msaidizi wa Polisi Mohamed Mpinga, Mkurugenzi wa Radio One Stereo, Deogratius Rweyunga kuhusiana na kampeni ya kuzuia ajali barabarani inayojulikana kama“Zuia Ajali Sasa,Toa Taarifa Mapema” kupitia namba 0800757575.Kampeni hiyo inaendeshwa na jeshi la polisi  kikosi cha Usalama barabarani,Vodacom Tanzania na kwa vyombo vya habari vya kampuni ya IPP .
 Mkuu wa jeshi la polisi kikosi cha Usalama Barabarani Kamanda Mohamed Mpinga (kulia) akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia (kushoto) kuhusiana na  kampeni ya kuzuia ajali barabarani inayojulikana kama“Zuia Ajali Sasa,Toa Taarifa Mapema” kupitia namba 0800757575,Katikati ni Mkurugenzi wa Radio One Stereo, Deogratius Rweyunga.Kampeni hiyo inaendeshwa na jeshi la polisi  kikosi cha Usalama barabarani,Vodacom Tanzania  na Vyombo vya habari vinavyomilikiwa na kampuni ya IPP .
Mkurugenzi wa Radio One Stereo, Deogratius Rweyunga(katikati)akishuhudiwa na Mkuu wa jeshi la polisi kikosi cha Usalama Barabarani Kamanda Mohamed Mpinga(kushoto) Rosalynn Mworia Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania akibandika stika yenye namba 0800757575 ambayo imetolewa mahususi kwa abiria wanaotumia vyombo vya moto kusafiria kutoa taarifa bure kupitia namba hizo wakati wa uzinduzi wa kampeni inayojulikana kama “Zuia Ajali Sasa,Toa Taarifa Mapema” Kampeni hiyo inaendeshwa kwa usirikiano baina ya  Jeshi la Polisi  kikosi cha Usalama barabarani,Vodacom Tanzania na vyomo vya habari vinavyomilikwa na kampuni ya  IPP.


TANZANIA HOME EXPO KUFANYA MAONYESHO YA 5 JIJINI DAR

Na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.
KAMPUNI ya Tanzania Home Expo inatarajia kufanya maonyesho ya bidhaa zake  mbalimbali katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City jijini Dar es Salaam,Mei 3o hadi Juni mosi mwaka huu.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Tanzania Home Expo,Zenno Ngowi wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya habari MAELEZO leo jijini Dar es Salaam.

Ngowi  amesema kuwa katika maonyesho hayo ya  matano ,Wananchi wajitokeze  kwa wingi ili kujua nini wanafanya na pia ni namna gani mikopo ya nyumba inaweza kupatikana kwa urahisi na kwa gharama  nafuu, kwakuwa katika maonyesho hayo kutakuwa na watu wanaotoa elimu juu ya mikopo nafuu.

Ameongeza kuwa watatoa elimu na njia ya upatikanaji wa nishati mbadala,ujenzi nafuu na uendelezaji wa upatikanaji wa makazi bila gharama yeyote.
Mkurugenzi Mkuu wa Tanzania Home Expo,Zenno Ngowi akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa idara ya Habari MAELEZO leo jijini Dar es Salaam kuhusiana na wananchi wajitokeze kwenye maonyesho ya 5 ya Tanzania Home Expo, ambapo kutaonyeshwa jinsi wanavyo fanya kazi na namna mbalimbali ambazo wanaweza kupata mikopo ya nyumba kwa bei rahisi kutoka kwenye mabenki mbalimbali hapa nchini, kushoto ni Afisa Masoko wa EAG Group Ltd Helen Mangare na Kulia ni Afisa Masoko wa EAG Group Ltd, Richard Raymond.
Baadhi ya waandishi wa habari walio hudhuria katika mkutano wa kuhamasisha wananchi kwenda kwenye maonyesho ya 5 ya Tanzania Home Expo yatakayofanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam kuanzia ijumaa wiki hii. PICHA NA EMMANUEL MASSAKA,GLOBU YA JAMII


WAZIRI MKUU PINDA APOKEA VITABU KUCHANGIA SHULE ALIYOSOMAWAZIRI MKUU Mizengo Pinda amepokea msaada wa vitabu 895 vyenye thamani ya sh. milioni 6.5/- ikiwa ni jitihada ya wadau mbalimbali kuchangia shule ya msingi aliyosoma ya Kakuni iliyoko kijiji cha Kibaoni, wilayani Mlele, mkoani Katavi.Waziri Mkuu amepokea msaada huo jana mchana (Jumanne, Mei 26, 2015) kwenye shule mpya ya msingi Kakuni ambayo bado inaendelea kujengwa kwenye kijiji cha Kibaoni.Akizungumza katika hafla hiyo fupi mara baada ya kupokea msaada huo, Waziri Mkuu Pinda aliishukuru kampuni ya General Booksellers Ltd ya kutoka Dar es Salaam kwa msaada huo ambao alisema utachangia kwa kiasi kikubwa kuitimiza ndoto yake aliyokuwa nayo ya kuisaidia jamii iliyomsomesha.“Wazo la ujenzi wa shule mpya ya msingi Kibaoni lilitokana na ukweli kwamba nilisoma na kumaliza kwenye shule hii ya Kakuni. Nikiwa ni mtumishi wa Serikali, ni Mbunge na sasa hivi ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nilijiuliza hivi shule hii ninaweza kuiacha hivi hivi?”“Nilijiuliza sana ni jambo gani ambalo naweza kulifanya la kusaidia wanakijiji wenzangu na kata nzima ya Kibaoni kama shukrani kwa kunilea na kunifikisha hapa nilipo. Ndipo wazo la kujenga shule niliyosoma likazaliwa kama mwaka mmoja na nusu uliopita,” alisema Waziri Mkuu wakati akiwahutubia wazazi, walimu na wanafunzi.

ZAIDI SOMA HAPAKIKAO CHA MAAFISA WAANDAMIZI WA JESHI LA MAGEREZA NCHINI CHAANZA LEO MKOANI MOROGORO

  Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil akitoa hotuba ya ufunguzi leo Mei 26, 2015 kwenye Kikao cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza nchini kinachofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Edema, Mkoani Morogoro.
  Wajumbe wa Kikao ambao ni  Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza nchiniwa kifuatilia kwa makini hotuba ya Mgeni rasmi, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil(wa kwanza kushoto) ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Magereza Joel Bukuku.
  Mshauri Mwelekezi katika Maboresho ndani ya Jeshi la Magereza Nchini, Dkt. Haji Semboja kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akiwasilisha Mada ya Maboresho ndani ya Jeshi la Magereza kwa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza nchini.
 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, John Casmir Minja(kushoto) akiteta jambo na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil kwenye kikao  cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza nchini kinachofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Edema, Mkoani Morogoro.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil(shati jeupe) akiwa kwenye picha ya pamoja na Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza nchini waliosimama nyuma(wa sita kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, John Casmir Minja(wa tano kushoto) ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa Magereza, Gaston Sanga(wa tatu kulia) ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Leonard Paul(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).