Na.
Catherine Sungura.
Wazazi
nchini wametakiwa kuwakinga watoto wao wakati waendeshapo magari kwa
kuhakikisha wanawafunga mikanda ili kuwaepusha na ajali za barabarani na
kudhibiti madhara yatokanayo na ajali.
Rai hiyo
imetolewa leo jijini hapa na kaimu kamanda
kikosi cha usalama barabarani Tanzania,Kamishna Msaidizi wa Polisi Fortunatus
Musilimu wakati akifungua mafunzo kwa Mawakili,Mahakimu ,Waendesha
Mashitaka na Askari wapelelezi wa kesi za ajali za barabarani,iliyoandaliwa na
wizara ya afya kwa kushirikiana na shirika la Afya Duniani (WHO) kupitia mpango
wa Bloomberg Initiative Global Road Safety.
Alisema
wazazi wengi wanapokuwa wanaendesha magari hawawafungi mikanda watoto wao na
hivyo ajali inapotokea watoto wanakuwa ni wahanga wakubwa kwa kupoteza maisha
au kupata ulemavu wa kudumu
“Wazazi
mnawalindaje watoto,baba anaendesha gari,mtoto yupo kwenye usukani anaendesha
nae gari,hiyo siyo sahihi ,tuwalinde watoto wawe salama kwa kuvaa mikanda”
Aidha, Kamanda
Musilimu alisema tatizo la ajali
barabarani nchini imekua ikiongezeka kila mwaka na hii ni kutokana na wananchi
kutokuona kama ajali ni tatizo kubwa na la haraka ambalo linafanya kuongezeka
kwa vifo nchini kulinganisha na magonjwa mengine na hivyo kupoteza nguvu kazi
ya taifa kiuchumi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...