Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Waziri wa Biashara na Viwanda wa Urusi Mhe. Denis Manturov aliyeongoza ujumbe maalum kutoka kwa Rais wa Urusi Mhe. Vladmir Putin wakati ujumbe huo ulipofika Ikulu Dar es salaam April 28, 2016. Katika mazungumzo yao Viongozi hao wamezungumzia kuhusu kuendelea kuzidisha ushirikiano katika Nyanja mbalimbali za kimaendeleo baina ya Tanzania na Urusi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Waziri wa Biashara na Viwanda wa Urusi Mhe. Denis Manturov aliyeongoza ujumbe maalum kutoka kwa Rais wa Urusi Mhe. Vladmir Putin wakati ujumbe huo ulipofika Ikulu Dar es salaam April 28, 2016. Katika mazungumzo yao Viongozi hao wamezungumzia kuhusu kuendelea kuzidisha ushirikiano katika Nyanja mbalimbali za kimaendeleo baina ya Tanzania na Urusi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, katikati akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Biashara na Viwanda wa Urusi Mhe. Denis Manturov aliyeongoza ujumbe maalum kutoka kwa Rais wa Urusi Mhe. Vladmir Putin wakati ujumbe huo ulipofika Ikulu Dar es salaam April 28, 2016. Katika mazungumzo yao Viongozi hao wamezungumzia kuhusu kuendelea kuzidisha ushirikiano katika Nyanja mbalimbali za kimaendeleo baina ya Tanzania na Urusi.(Picha na OMR)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Ila nimehuzunishwa na kusikitishwa sana khususan kwa baadhi ya picha miongoni mwa hizo zikisambaa na kuonyesha jambo ambalo sio la kiutu, uungwana, heshma, ustaarabu wala maadili ya utamaduni wetu. Pia ni kujidhalilisha sisi wenyewe na kuonyesha ni jinsi gani tunakosa alau ule utu tu iwapo uzalendo umeshindikana. Nadhani ifike wakati khususan hao wapiga picha wetu (wanakhabari kwa jumla) au hao wanaohusika na upigaji picha katika ngazi hizo za viongozi wetu wa juu, nadhani baadhi ya dosari zinapojidhihirisha au kujitokeza kwa namna moja ama nyingine, hebu tutumie utu na uzalendo wetu kuzirekebisha na ikibidi kustiri jambo hilo au lolote husika ambalo kiubinaadam, kiuungwana, kiustaarabu, kimaadili na kubwa kiutu laweza kumkwaza muhusika zaidi, kumdhalilisha na hata kutudhalilisha wananchi wote kwa jumla, sio busara pale tunaporuhusu kusambaza all over the place. Na ikikibidi kupatikana wahusika wa masuala kama hayo, basi hatua husika zichukuliwe ile kukomesha kabisa tabia na matukio kama hayo ya kuwadhalilisha viongozi wetu khususan wanapoghafilika au kutokezewa na dharura au mambo ya kiubinaadam, leo yaweza kuwa kwa yule kesho ikawa kwako au kwangu mimi na hata mwengine yeyote yule, utu tuutangulize mwanzo, kwani hata fakhari sometimes ni mama wa ujinga.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...