Kaka Michuzi napongeza kwa idea yako hii, ni kweli sisi wananchi ndio tunaotakiwa tuonyeshe kero zetu. Leo nakuja na hili suala la kuweka dampo la taka katikati ya makazi ya watu.

Hapa Temeke mwisho jijini Dar es salam kuna Dampo la taka kuubwa limewekwa katikati ya makazi ya watu . sababu ya dampo hili kuwepo hapo mpaka sasa hatujui.Madhara ya dampo hili ni makubwa kuliko faida zake.Kwa mfano wakati huu wa mvua dampo hili limekua likitoa harufu mbaya inayokera sana sisi wakazi, Dampo limekua ni mazalio ya inzi na kusababisha kipindu pindu.

Je nauliza viongozi wa Manispaa ya temeke hawalijui hili, au wanasubiri mpaka kiongozi mkubwa awatembelee ndio atoe amri ya nini kifanyake.

Naambatanisha picha uone hali halisi mjionee Kijipu Upele hiki cha huku kwetu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Wameanza kuzoa usikuu huu

    ReplyDelete
  2. Nilikuwa Tanzania wiki mbili zilizopita, nilibahatika kupita maeneo Ya TMK, ni kweli nililiona hili jalala, nikajiuliza, Kulikoni ?!! Ni aibu sana kukaa karibu na UCHAFU! HATARI sana.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...