Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mahandisi, Isack Kamwela akijibu swali la Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea leo Bungeni mjini Dodoma alilotaka kujua ni lini Serikali itamaliza tatizo sugu la maji katika Jiji la Dar es salaam. 
  Naibu waziri ofisi ya waziri Mkuu Mkuu Sera, kazi, Ajira, Bunge, Vijana na walemavu Dkt. Abdallah Possi akijibu la Stella Ikupa Alex (Viti Maalum) alitaka kujua upatikanaji wa zabuni za kazi kwa watu wenye ulemavu leo Bungeni mjini Dodoma.
(Picha na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Dodoma. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akiteta na Mbunge  wa Ilala  Azzan  Mussa Zungu, bungeni mjini Dodoma Aprili 29, 2016.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Na Eleuteri Mangi-MAELEZO, Dodoma.
SERIKALI itaendelea kutekeleza ahadi zake ilizoahidi ya kuwapatia maji wananchi wake ikiwemo wakazi wa jiji la Dar es salaam ili kutatua adha ya maji inawakabili katika maenneo yao. 

Kauli hiyo imetolewa leo Bungeni mjini na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mahandisi Isack Kamwela wakati akijibu swali lililoulizwa na Mbunge wa Ubungo jijini Dar es salaam Saed Kubenea lenye vipengele (a), (b), na (c) lililohoji ni lini Serikali itamaliza tatizo sugu la maji katika Jiji la Dar es salaam.

Mahandisi Kamwela amesema kuwa Serikali imekamilika na kufanikisha upatikanaji wa maji katika jiji la Dar es salaam kwa kuongeza uzalishaji wa maji kutoka mtambo wa Ruvu Chini na ulazaji wa bomba kubwa lenye kipenyo cha mm 1800 kutoka Ruvu Chini hadi Dar es salaam lenye urefu wa km 56.

“Hali ya upatikanaji wa maji katika jiji la Dar es salaam inaendelea kuimarika kwa kuzingatia kuongzeka kwa uzalishaji maji kutoka Ruvu Chini ambao una uwezo wa kuzalisha lita milioni 270 za maji kutoka lita milioni 180 za awali kwa siku” alisema Mahandisi Kamwela.  

Katika kuhakikisha jiji hilo linakuwa na maji ya kutosha kwa wakazi wake, Mahandisi Kamwela amesema kuwa mradi wa upanuzi wa Ruvu Juu nao umekamilika na una uwezo wa kutoa maji lita milioni 196 kutoka lita milioni 82 za awali kwa siku.

Ili kuhakikisha maji yanawafikia walengwa, Mahandisi Kamwela kazi za ulazaji za ulazaji wa mabomba mawili kutoka Mlandizi hadi Kimara, ujenzi wa tenki jipya la maji eneo la Kibamba na ukarabati wa matenki ya Kimara zimefikia wastani wa asilimia 98, hatua hiyo imewezesha majaribio ya uendeshaji wa mitambo hiyo kuanza mapema Aprili mwaka huu.

Aidha,  Mahandisi Kamwela amesema kuwa Serikali inaendelea kutekeleza mradi wa Kimbiji na Mpera  ambapo hadi sasa mkandarasi amekamilisha uchimbaji wa visima tisa kati ya visima 20 ambapo kazi hiyo inatarajiwa kukamilika mwezi Agosti mwaka huu, hadi kukamilika visima hivyo vitakuwa na uwezo wa kuzalisha maji lita milioni 260 kwa siku. 

Hadi sasa uzalishaji wa maji katika jiji hilo umefikia lita milioni 390 kwa siku ikilinganishwa na mahitaji ya lita milioni 450 ya sasa.

Akijibu swali la nyongeza la Kubenea alioitaka kujua maeneo yatakayonufaika na miradi hiyo ya maji, Mhandisi  Kamwela ameyataja maeneo hayo yatakayonufaika ni pamoja na maeneo ya uwekezaji (EPZ) Bagamoyo, Chasimba, Buma, Zinga, Kerege na Mpiji mkoa wa Pwani.

Maeneo mengine yatakayonufaika na mradi huo kwa Mkoa wa Dar es salaam ni Bunju, Wazo, Salasala, Madale na Kinzudi Mbezi Juu, Goba, Kawe, Makongo, Mwenge, Msasani, Mikocheni, Mlalakua, Masaki, Sinza, kijitonyama, Manzese, Konondoni, Magomeni, Kigogo, Vingunguti, Buguruni, Kariakoo na Ilala kwa upande wa Ruvu Chini wakati Mtambo wa Ruvu Juu utawahakishia wakazi wa maeneo Mlandizi, Kibaha, Kibamba, Mbezi, Kimara, Ubungo, Kibangu, Makuburi pamoja na eneo lote la Tabata.

Kukamilika kwa miradi yote itaongeza uzalishaji na upatikanaji wa maji katika jiji la Dar es salaam hadi kufikia lita milioni 750 ambayo yatakidhi mahitaji ya wakazi hao hadi kufikia mwaka 2032.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...