Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imepatiwa msaada wa vifaa kumi  vya tiba vya kuwahudumia watoto  mara wapougua na kufikishwa kwenye hospitali hiyo.

Vifaa hivyo vina thamani ya Dola za Kimarekani Laki moja sawa na zaidi Sh milioni 200 vimetolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF),kwa lengo la kupunguza vifo vya watoto walio chini ya umri wa miaka mitano.

Baadhi ya vifaa vilivyotolewa  ni Ventilator, medical, adult –child ,w/access pamoja na Warmer system , newborn, radiant, w/access.

Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo  Mwakilishi wa UNICEF Tanzania Dk Jama Gulaid amesema mchango wa UNICEF na michango ya wadau wengine itawezesha watumishi wa hospitali ya Muhimbili kuokoa maisha ya  watoto  ambao wanahitaji huduma za afya.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Donan Mmbando  amesema  hadi kufikia mwaka 2013  Tanzania imefanikiwa kupunguza vifo vya watoto hao kwa theluthi mbili.

Kwa mujibu wa Dk Mmbando, mwaka 2013 Tanzania imepunguza vifo hivyo na kufikia 54 kwa vizazi hai 1,000  na kufikia lengo la Milenia  na kwamba  mafanikio hayo yametokana na kiwango kikubwa cha chanjo , matumizi sahihi  ya dawa za Malaria pamoja na vyandarua.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Profesa Lawrence Mseru amewashukuru UNICEF kwa msaada huo ambao utachangia kwa kiasi kikubwa kuokoa maisha ya watoto na kuboresha huduma za afya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...