Mwanafunzi Revotha Selestine (Mwenye kinasa Sauti) akitoa shukrani kwa niaba ya wanafunzi wenzake katika Maadhimisho ya Siku ya Posta Duniani yaliyoadhimishwa jana Octoba 09,2015 kwa ngazi ya Mkoa wa Mwanza katika Jiji la Mwanza zilipo ofisi za Shirika la Posta Mkoani Mwanza.

Na:George Binagi-GB Pazzo
Katika Shindano la Uandishi wa Barua lililoshirikisha wanafunzi zaidi ya 2,000 nchi nzima, aliibuka mshindi wa nne Kitaifa huku mshindi wa pili pia kitaifa akitokea Mkoani Mwanza.

Katika shindano hilo lililokuwa na kichwa cha habari kisema "Tueleze kuhusu dunia ambayo ungependa kuiishi", Mkoa wa Mwanza ulitoa washindi watano kati ya 10 Kitaifa na hivyo kuibuka kidedea katika shindano hilo na kufuatiwa na Mkoa wa Tanga.

Washindi kumi wa shindano hilo ni Irene Ambrose Gindo (Kifungilo Girls Secondary School-Tanga), Anitha Mutembukwa (St.Joseph Girls School-Mwanza), Anna Godlove (Kifungilo Girls Secondary School-Tanga), Revotha Selestine (St.Joseph Girls Secondary School-Mwanza) na Victoria Nsajigwa Mbije (Kifungilo Girls Secondary School-Tanga).

Wengine ni Careen Edwin Mlay (St.Marry's Mazinde Juu Secondary School-Tanga), Richard Samwel Yadoma (Buswelu Secondary School-Mwanza), Miriam Amini Msuya (St.Marry's Mazinde Juu Secondary School-Tanga), Febronia Mkama (St.Joseph Girl's Secondary School-Mwanza) pamoja na Angela Ananias (St.Joseph Girls Secondary School-Mwanza) ambapo katika ya washindi hao kumi, mvulana ni mmoja tu.

Siku ya Posta duniani ilianza kuadhimishwa na nchi mwanachama wa jumuiya ya Umoja wa Mataifa tangu mwaka 1874 ambapo Tanzania ilijiunga na umoja huo tangu mwaka 1963.
Kutoka Kushoto ni Mkuu wa Shule ya Sekondari St.Joseph Girls ya Mkoani Mwanza Agnes Medard, Mwakilishi wa Mgeni rasmi Afisa Elimu Mkoa wa Mwanza Baseki Josephat Sheja, Meneja wa Shirika la Posta Mkoa wa Mwanza Julius Chifungo pamoja na Mwakilishi wa Mkuu wa Shule ya Sekondari Buswelu ya Mkoani Mwanza Mwl.Ruth Maboto
Kutoka Kushoto ni Mkuu wa Shule ya Sekondari St.Joseph Girls ya Mkoani Mwanza Agnes Medard, Mwakilishi wa Mgeni rasmi Afisa Elimu Mkoa wa Mwanza Baseki Josephat Sheja pamoja na Meneja wa Shirika la Posta Mkoa wa Mwanza Julius Chifungo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...