Mahmoud Ahmad Arusha
WATANZANIA
500,000 wanatarajiwa kutembelea mbuga zote 16 za hifadhi za taifa mwaka
huu ikiwa ni hatua ya kuimarisha na kukuza utalii wa ndani ambapo
watajionea vivutio mbalimbali vilivyomo ndani ya hifadhi hizo.
Hayo
yameelezwa leo na Meneja uhusiano wa shirika la hifadhi za taifa,
Tanapa, (Pichani)Pascol Shelutete, makao makuu ya TANAPA, jijini ,Arusha,
alipokuwa akizindua hatua ya mwisho ya kampeni maalumu ya miezi sita
ya kuhamasisha Watanzania kutembelea hifadhi ili kujionea vivutio
kwenye hifadhi wanazopakana nazo ili kuimarisha utalii wa ndani
Kampeni
hiyo ni Makakati maalumu uliobuniwa na Tanapa, unaotoa hamasa kwa
watanzania kutembelea mbuga za hifadhi zilizopo karibu na maeneo yao kwa
gharama nafuu hasa siku za mwishoni mwa wiki na hivyo kuwapunguzia
matumizi ya fedha wanazotumia kwenye starehe na badala yake wazitumie
kutembelea hifadhi .
Meneja
uhusiano wa Tanapa, Shelutete, amesema kuwa kadiri miaka inavyozidi
kusonga mbele mwamko wa watanzania kutembelea mbuga za hifadhi
unaongezeka, ambapo mwaka 2013 watanzania 362,217, walitembelea hifadhi
zote 16 nchini, na mwaka 2014 watanzania 427,258 wametembelea mbuga hizo
.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...