Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilipokea Rufaa za Wabunge 55 na imeshatolea maamuzi rufaa 42  bado rufaa za Wabunge 13 ambazo vielelezo vyake vinasubiriwa kutoka kwenye Halmashauri husika. 
Kulikuwa na Rufaa 16 za Wabunge waliokuwa wameenguliwa. Kati ya hizo Wabunge 13 wamerudishwa kuendelea na kampeni na rufaa 3 Tume ilikubaliana na maamuzi ya Wasimamizi wa Uchaguzi hivyo hao hawatarudishwa kwenye orodha ya Wagombea. 
Aidha, rufaa 24 zimekataliwa na Tume ambapo maamuzi ya Wasimamizi wa Uchaguzi yataendelea kubaki kama yalivyo na wagombea wataendelea kugombea. Pia kuna rufaa 2 ambazo Tume haijazijadili kwa kuwa hazikufuata utaratibu wa kuwasilisha Tume yaani kupitia kwa Wasimamizi wa Uchaguzi wa Majimbo husika hivyo, maamuzi ya Wasimamizi wa Uchaguzi yatabaki kama yalivyo na wagombea wataendelea kugombea kama walivyoteuliwa. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...