Bwn. Daniel Korona akisherehesha hafla fupi ya kumuaga Balozi wa Umoja wa Afrika aliyemaliza muda wake Mhe. Amina Salum Ali iliyoandaliwa na Jumuiya ya Diaspora kutoka Afrika wanaoishi Montgomery county iliyofanyika siku ya Jumatano Sept 2, 2015 Silver Spring, Maryland.
Kulia ni mwongozaji maswali Bi. Soffie Ceesay ambaye ni mwanachama mwanzilishi wa Montgomery County's African Affairs Advisory Group na African Immigrant Caucus akimuuliza Mhe. Amina Salum Ali maswali mbalimbali likiwemo nini anajivunia kwenye uongozi wake kama Balozi wa kwanza wa Umoja wa Afrika nchini Marekani. Balozi Amina Salum Ali alieleza ni ushirikiano wa nyanja mbalimbali mabalozi nchi za Afrika zimenufaika na kupata mafanikio na uhusiano wa AU na Marekani kwa kuwezesha kupata Balozi wao nchini Marekani na kikubwa kabisa katika historia ya AU na yeye  kama Balozi kuwezesha Rais Barack Obama kwa mara ya kwanza katika historia kama Rais wa Marekani kuhutubia Umoja huo.
Isiah Leggett ambaye ni Montgomery County Executive akimtunukia cheti Mhe. Balozi Amina Salum Ali

KWA PICHA ZAIDI OFYA HAPA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hongera balozi uweza wako wa kuongoza bado unatakiwa andika kitabu kuhusu bara hili na mawazo yako kuhusu jinsi ya kulikwamua kiuchumi kwa manufaa yetu na vizazi vijavyo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...