BWANA NASIFU AHMED LEMA

MTAJWA HAPO JUU NI RAIA WA TANZANIA AMBAYE KWA SASA YUKO AFRIKA KUSINI. BW. LEMA ANA HALI MBAYA KIMAISHA. ANADAI KWAMA ALIZALIWA HIMO MAKUYUNI KIJIJI CHA LOTIMA MKOANI KILIMANJARO MWAKA 1968. WAZAZI WAKE NI AHMED LEMA NA ANNA MFINANGA AMBAO KWA SASA WOTE NI MAREHEMU.


UBALOZI WA TANZANIA AFRIKA KUSINI UNAOMBA KAMA KUNA YOYOTE AMBAYE ANAWAFAHAMU NDUGU ZAKE WAPATIWE TAARIFA HII.
WANAWEZA KUWASILIANA NA UBALOZI KITENGO CHA UHAMIAJI KWA NAMBA ZIFUATAZO: +27 12 342 4371 AU +27 12 342 4393

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Pole sana kwa ndugu Nasif Ahmed..

    Hivi balozi zetu nchi za nje hazina namna/utaratibu wa kuwasaidia raia wa Tanzania wanaopatwa na matatizo kama ya ndugu huyo ambapo hakuna ndugu? Nimelazimika kuuliza swali hilo maana maelezo yapo wazo hapo kwenye habari kuwa wazazi wake wote ni marehemu.

    ReplyDelete
  2. Tunataka mabadiliko mpaka kwa hizi balozi hawana msaada yoyote. Wanakula pesa tu na chuki zimejaa Yani hata ukienda wanakuzarau na kweli. Wamejaaa wahindi na wengineo

    ReplyDelete
  3. Mimi nilikua nafikiria kazi ya ubalozi ni pamoja na kuwasaidia wananchi wake wenye matatizo kama ya huyo kijana.

    ReplyDelete
  4. Kwani ubalozi wa Tanzania kumsaidia huyo mtu mmoja mnaona mtafilisika? Acheni roho mbaya nyie.

    ReplyDelete
  5. Yaani wewe uende nje kutafuta maisha yakushinde halafu utegemee fedha za walipa kodi zikusaidie wakati hapa Tanzania kuna watu wenye matatizo makubwa kuliko ya huyu na hawasaidiwi! Hela zilizoko kwenye ubalozi ni za walipa kodi na zinatakiwa zisaidie WAGONJWA TU. Kama kila aliyekwama maisha huko MAJUU atasaidiwa na ubalozi watasaidiwa wangapi na kwa vigezo gani? Huyu ameomba ndugu zake wamsaidie na kama hawakuonekana mfuko wa Tanzania walioko huko inabidi utumike kumsaidia lakini si FEDHA ZA WALIPA KODI.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...