MBUNGE wa Sengerema mkoani Mwanza, William Ngeleja akibadilisha mawazo na wabunge wenzake, Ezekiel Maige (Msalala) na Dk. Dalaly Peter Kafumu (Igunga), wakati aliporejesha fomu kwenye ofisi za Makao Makuu ya CCM, mjini Dodoma.
MBUNGE wa Sengerema mkoani Mwanza, William Ngeleja, akirejesha fomu za kuomba kuteuliwa kuwania urais kupitia CCM kwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Rajab Luhwavi, kwenye Ofisi za Makao Makuu ya Chama hicho mjini Dodoma, jana.

Na Mwandishi Maalum, Dodoma

MBUNGE wa Sengerema, William Ngeleja, amesema amepata fundisho kubwa katika harakati zake za kuwaomba udhamini ili ateuliwe kuwania urais na kwamba, limemuongezea shauku kubwa ya uongozi.

Ngeleja, ambaye amepata kuwa Waziri wa Nishati na Madini katika serikali ya Awamu ya Nne chini ya Rais Jakaya Kikwete, amesema yuko tayari kuwatumikia watanzania iwapo CCM kitampa ridhaa ya kupeperusha bendera.

Akizungumza wakati akirejesha fomu za kuomba kuwania urais kwenye uchaguzi mkuu ujao, Ngeleja alisema anatambua nafasi anayoimba ni nyeti na kwamba, amejipima na anatosha kubeba mikoba ya JK.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...