Mwakilishi wa Jimbo la Rahaleo Mhe Nassor Salim Jazira akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi Vifaa kwa Wananchi wa Jimbo lake iliofanyika katika Skuli ya Msingi Rahaleo Zanzibar.
Waziri wa Uwezeshaji Ustawi wa Jamii Vijana Wanawake na Watoto Mhe. Zainab Omar, akizungumza na Wananchi wa Jimbo la Rahaleo na wanafunzi wa skuli hiyo katika hafla ya kukabidhi vifaa vilivyotolewa na Mwakilishi wa Jimbo hilo Mhe. Nassor Salim Jazira.
Waziri wa Uwezeshaji Ustawi wa Jamii Vijana Wanawake na Watoto Mhe Zainab Omar akimkabidhi Seti ya Komputer Mwanafunzi wa Chuo cha Ualimu Rahaleo,kwa ajili ya matumizi ya Chuo hicho vilivyotolewa na Mwakilishi wa Jimbo la Rahaleo Mhe Nassor Salim Jazira, hafla hiyo ya makabidhiano imefanyika katika Skuli ya Rahaleo.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 02, 2015

    Hata mwanangu leo kaniuliza na umri wa miaka mitano kwa nini vifaa vya michezo na kazi nyingine vinatolewa na wabunge/wawakilishi kwa wingi mwezi huu. ilibidi nimfundishe somo la siasa kwa nini waheshimiwa wako bize kutowa misaada kwa wananchi hii sio rushwa hii ni miezi ya riziki ukikupita msimu huu wa mavuno iko haja ya kusubiri tena miaka mitano ijayo shughuli zote za maedeleo husitishwa mpaka tukaribie uchaguzi ndio kazi huanza kweli tutafika tunapo taka kwenda ikiwa ufanyaji kazi ni wa misimu.

    asante.
    mchunguzi wa kujitolea.

    saedy mavuzy,zanzibar.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...