THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512,
2116898
E-mail: ikulucommpress@googlemail.com
Fax: 255-22-2113425 |
|
PRESIDENT’S OFFICE,
STATE
HOUSE,
1 BARACK OBAMA ROAD,
11400
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amepokea
kwa masikitiko na huzuni nyingi taarifa ya kifo cha mwanasiasa mkongwe nchini
na aliyepigania uhuru wa Tanganyika, Ndugu Samwel Ntambala Ruangisa, ambaye
aliaga dunia mwanzoni mwa wiki hii nchini Marekani ambako alikuwa anatibiwa.
Katika
salamu za rambirambi ambazo amempelekea Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Mheshimiwa John
Mongella kuomboleza kifo cha Mzee Ruangisa, ambaye pia alikuwa bado diwani
katika Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba, Rais Kikwete amesema:
“Nimepokea
taarifa za kifo cha Mzee Ruangisa kwa masikitiko na huzuni nyingi. Kwa zaidi ya
nusu karne, Mzee Ruangisa amekuwa kiongozi wa kuigwa mfano katika nafasi zote
ambazo zimepata kuzishikilia katika maisha yake kuanzia Ukuu wa Mkoa wa Ziwa
Magharibi (sasa Kagera) na baadaye Mkoa wa Mara tu baada ya Uhuru wa Tanganyika
mwaka 1961, Ubalozi, Uwaziri, Ubunge, Umeya na Udiwani. Katika kila nafasi aliyoishikilia,
Mzee Ruangisa alionyesha uongozi wa kiwango cha juu. Kwa hakika, tumepoteza
kisima cha uzoefu wa uongozi.”
Rais
Kikwete ameongeza katika salamu zake za rambirambi: “Mkuu wa Mkoa nakutumia salamu
zangu za rambirambi kuomboleza msiba huu na kupitia kwako naomba uwape pole
wana-Kagera wote kwa kuondokewa na mzee wao wa siku nyingi.
Aidha, naomba
unifikishe pole zangu nyingi kwa wanafamilia wote ambao wamepoteza baba, babu
na mhimili wa familia. Wajulishe kuwa niko nao katika kipindi hiki kigumu.
Waambie naelewa machungu yao kwa sababu machungu yao ni machungu yangu. Vile
vile, naungana nao katika kumwomba Mwenyeji Mungu, Mwingi wa Rehema, aiweke
peponi roho ya Marehemu Samwel Ntambala Ruangisa. Amina.”
Imetolewa na;
Kurugenzi ya
Mawasiliano ya Rais,
IKULU,
DAR ES SALAAM.
27 Mei, 2015
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...