Mshindi wa kitita cha shilingi milioni 100/- kupitia promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania, Irene Mrema (kushoto) mkazi wa Kawe Jijijini Dar es Salaam akifafanua jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa hafla ya kukabidhiwa hundi yake na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia (katikati) na Balozi wa promosheni hiyo Hillary Daud”Jaymillions”kulia baada ya kuibuka mshindi wa kitita hicho kupitia promosheni hiyo ambayo imeongezwa muda mpaka Mei 7 mwaka huu.Hafla hiyo ilifanyika makao makuu ya kampuni hiyo Mlimani City jijini Dar es Salaam. Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno JAY au AUTO kwenda namba 15544.
Balozi wa Promosheni ya JayMillions Hillary Daud”Jaymillions”(kushoto)akimkabidhi hundi yenye thamani ya shilingi milioni 100/- Mshindi wa kitita hicho mkazi wa Kawe jijini Dar es salaam Irene Mrema(kulia) alichojishindia kupitia promosheni hiyo inayoendeshwa na Vodacom Tanzania, anayeshuhudia katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa kampuni hiyo, Rosalynn Mworia.Hafla hiyo ilifanyika makao makuu ya kampuni hiyo mlimani city jijini Dar es Salaam. Mlimani City jijini Dar es Salaam. Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno JAY au AUTO kwenda namba 15544.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Hongera Irene kwa kuwa mmoja kati ya mamilionea wanaoongezeka, ukishapokea kitita chako jipange kuboresha maisha yako na jamii yako. La muhimu zaidi kama unataka kuendelea kuwa kwenye ligi ya mamilionea kwa muda, wekeza katika mradi au uwekezaji mwingine wowote utakaoendelea kukupatia fedha.

    ReplyDelete
  2. Watu wanafanyafanyaje kupata pesa hiyo kutoka Jaymilionea? unachezaje huo mchezo mbona nami nautamani sana?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...