Kesho siku ya Jumamosi tarehe 25 Aprili, 2015, kuanzia saa 12:00 hadi saa 2:00 asubuhi, kutakuwa na zoezi la matembezi ya miguu kwa watumishi wa taasisi mbalimbali Mkoani Dodoma.


Matembezi hayo yataanzia viwanja vya bwalo la polisi Mjini Dodoma na kufuata uelekeo wa barabara ya Bunge la Tanzania, Barabara ya Dodoma Inn, Mtaa wa Nyerere na kurudi viwanja vya Bwalo la Polisi ambapo ndio kituo cha mwisho. 
Matembezi hayo yataongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Gallawa. Vilevile yatahudhuriwa na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dodoma. 
Watumishi wa taasisi mbalimbali za Mkoani Dodoma wamealikwa kuhudhuria matembezi hayo. Taasisi hizo ni pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama kama Jeshi la Polisi, Magereza, JWTZ, JKT, Uhamiaji na Majeshi ya Akiba. Taasisi nyingine ni kama TAKUKURU, Ofisi za Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma, Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu na Mamlaka ya Majisafi na usafi wa mazingira-DUWASA. Taasisi nyingine ni Mabenki, Wamachinga, TCCIA (M), Mifuko ya Hifadhi za Jamii, Tume ya Utumishi wa Maadili ya Umma na CWT. 
Zoezi hili la matembezi limeanzishwa kwa Malengo ya kutoa fursa kwa watumishi wa taasisi mbalimbali Mkoani Dodoma kujumuika kwa pamoja katika mazoezi ya kutembea na litakua zoezi endelevu. Matembezi haya yatakuwa yakitumika kuhamasisha masuala ya kimkoa na kitaifa na yatakuwa yakifanyika kila Jumamosi ya Kwanza na ya mwisho ya kila mwezi.

Imetolewa na:
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma
Aprili 24, 2015

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hongera sana Mhe. Hawa Galawa kwa wazo hilo natumani litafanywa liwe la kitaifa. Litasaidia networking na kuweka afya za watumishi wa umma.vizuri pamoja na kupiga vita vitambi. Hongereni sana Dodoma kwa uamuzi huo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...