Na Bakari Issa,Dar es Salaam

Maspika wa Bunge wa Afrika Mashariki wamekutana jijini Dar es Salaam ili kujadili masuala mbalimbali yanayozihusu nchi za Ukanda wa Afrika Mashariki likiwemo suala la Ugaidi pamoja na vurugu zinazotokea ,maendeleo hususan Barani Afrika.

Katika Mkutano huo wenye jina la ‘Jukwaa la Maspika wa Mabunge ya Afrika Mashariki’ulihuduliwa na Maspika wa nchi za Tanzania,Kenya,Uganda, Rwanda pamoja na Spika wa Bunge la Afrika Mashariki(EALA),Mhe.Daniel Kidega.

Akizungumza katika makutano huo,Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa mkutano huo,Mhe.Anne Makinda amesema mkutano huo una lengo la kuangalia maendeleo ya nchi za Afrika Mashariki pamoja na mambo mazuri yaliyoko katika nchi za Afrika Mashariki ikiwemo tabu kama suala la Ugaidi.

Spika wa Bunge la Uganda,Mhe.Rebecca Kadaga amesisitiza juu ya ushirikiano baina ya nchi za Afrika Mashariki ikiwa ni pamoja na kuweka mikakati na mipango juu ya ulinzi wa nchi za Afrika Mashariki.

Kwa upande wa Spika wa Bunge la Kenya,Mhe.Justine Muturi amewahasa wananchi wa Afrika kuhakikisha ulinzi na usalama wa nchi za Afrika Mashariki na kuwahasa vijana wa nchi hizo kutojihusisha na vikundi visivyofaa.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa mkutano wa Jukwaa la Maspika wa Mabunge ya Afrika Mashariki,Mhe.Anne Makinda (katikati) azungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya uwepo wa mkutano huo hapa nchini. Wengine pichani toka kulia ni Mh. Justine Muturi (Spika wa Bunge la Kenya), Mh. Rebecca Kadaga (Spika wa Bunge la Uganda), Mh. Donatille Mukabalisa (Spika wa Bunge la Rwanda) pamoja na Mh. Daniel Kidega (Spika wa Bunge la Afrika Mashariki).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...