Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Mhe. Patrick Luciano Tsere (kulia) akikabidhi  Dawa za Binadamu na Mahindi  kwa Bw. Paul Chiunguzeni, Katibu Mkuu na pia Kamishna  anayeshughulikia masuala ya Maafa aktika Ofisi ya Makamu wa Rais wa Malawi  ikiwa  ni sehemu ya msaada wa Tani 1,200 za Mahindi na Dawa za Binadamu zilizotolewa na Serikali ya Tanzania kwa nchi hiyo kufuatia mafuriko makubwa yaliyoikumba nchi hiyo mwezi Januari 2015. 
manajdhdfdufdhuf Bw. Paul Chiunguzeni, Katibu Mkuu na pia Kamishna anayeshughulikia masuala ya Maafa katika Ofisi ya Makamu wa Rais wa Malawi akitoa hotuba ya shukrani kwa Serikali ya Tanzania kwa msaada huo wa Mahindi na Dawa za Binadamu.
Mhe. Balozi Tsere akiwa katika picha ya pamoja na Bw. Chiunguzeni. Wengine katika picha ni Mwambata wa Jeshi katika Ubalozi wa Malawi nchini Tanzania, Ufulu Kalino (kushoto) akifuatiwa na Kanali Rugeumbiza kutoka JWTZ ambaye alikuwa msimamizi wa zoezi la usafirishaji wa msaada huo kutoka Tanzania na Luteni Kanali B.B. Kisinda (wa tatu kulia) kutoka JWTZ ambaye alikuwa Kiongozi wa Msafara pamoja na Makamanda wa JWTZ.

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...