Mwenyekiti  wa Tamasha la Pasaka, Alex Msama akifafanua jambo kwa waandishi wa habari jijini Dar es salaam jana (hawapo pichani) kuhusu maandalizi  ya tamasha hilo litakalofanyika Aprili 5, ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe. Kulia ni Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi, Jimmy Charles. (Picha na Francis Dande)
Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Jimmy Charles akifafanua jambo.

Na Mwandishi Wetu


WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Tamasha la Pasaka litakalofanyika Aprili 5 mwaka huu jijini Dar es Salaam.



Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam juzi, Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama alisema maandalizi ya tamasha hilo yamekamilika kwa asilimia 97 hivyo amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi siku hiyo.


Alisema wameshakamilisha maandalizi ya tamasha hilo, ila kinachosubiriwa ni waimbaji  wa kimataifa Ephraim Sekeleti wa Zambia, Ifeanyi Kelechi kutoka Uingereza, Rebeca Malope na Thori Mahlangu wote kutoka Afrika Kusini pamoja na Faustine Munishi ‘Malebo’ kuanza kuwasili nchini.

“Tamasha la mwaka huu litakuwa la aina yake kwani tutakata keki, kupiga fataki kama ishara ya kutakiana amani, upendo  na mshikamano na tutaiombea nchi yetu  kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika  Oktoba mwaka huu’’alisema Msama.

Msama aliongeza kuwa tamasha la mwaka huu litabeba ujumbe mahsusi wa ‘amani na upendo ndio amani kwa watanzania’, aidha tamasha hilo pia litatumika kupiga vita maauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi ‘Albino’

Aliongeza kuwa ukiachia mgeni Waziri Membe, pia wageni mashuhuri watahudhuria tamasho hilo akiwemo rais mstaafu ali Hassani Mwinyi ambalo linatimiza miaka 15 tangu kuanzishwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...