Hivi punde nimetoka Makumbusho ya Taifa na Nyumba ya Utamaduni iliyopo mkabala na Chuo cha Usimamizi wa Fedha  (IFM)  jijini Dar es salaam. Hapo kulikuwa na matukio makubwa mawili.  Moja la sherehe za siku ya wanawake na Nyingine kwenye viwanja ikiwahusisha wanafunzi wa shule mbali mbali.
Muda mfupi kabla sijaondoka kuna wanafunzi  wawili wa Jangwani Sekondari walidondoka na kupoteza fahamu mmoja akiwa ameng’ata ulimi babisa, Hali hii ya sintofahamu iliwashtua wengi waliokuwa  karibu na tukio hili. Ilikuwa ni wanafunzi wenyewe waliochukuwa jukuamu la kuwasaidia wenzao. Pembeni ya tukio hili la kusikitisha niliwaona viongozi wa Makumbusho wakiwa chini ya mti mkubwa wakizungumza mambo yao bila hata kushtuka na kutoa msaada.
Hii inasikitisha sana, Nimeona niufahamishe umma hasa wenye maeneo ya kukodisha kwa shughuli za kijamii, kwamba msipuuzie wateja wenu wanapopatwa na matatizo kama nilivyo shuhudia pale makumbusho ya Taifa. Kwa kweli ni aibu sana kwa uongozi wa hapo...Ni aibu kwa kuwa mabinti waliopoteza fahamu ni sawa na watoto wao tu, ukiachana na kuwa ni wateja wa Makumbusho.
Nawapongeza vijana wachache wa Makumbusho hiyo waliojitolea kwa moyo kusaidiana na wanafunzi hao kuhakikisha waathirika wanakimbizwa hospitali. Pia Mtangazaji Sauda Simba Kilumanga  ambaye alijitoa sana kama mama kuhakikisha wanafunzi hao wanapatiwa msaada. 
Mungu awabariki wote na ninawaombea Mungu wanafunzi waliopelekwa hospital wapone haraka.

Mimi Mdau wa Makumbusho ya Taifa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Ni ubinadamu kusaidiana wakati mtu akipatwa na shida kama hiyo ya kupoteza ufahamu..Tunashukuru kwa kutukumbusha kuwa na moyo wa kusaidiana katika dharura kama hizi..

    ReplyDelete
  2. Si hayo tu mdau wa Makumbusho ya Taifa! Mimi pia ni mdau mkubwa pale, ila kinachoendelea hapo mahala kama serikali haijtupia jicho, mambo yatakuwa mabaya zaidi. Yaani kuanzia mapokezi kuna kina mama wanene hivi wajeuri ajabu. Unakwenda makumbusho unahudumiwa kama unaenda kuomba kazi pale! Umeona wapi mapokezi kuna watu wanne wote wakisimamia daftari la wanaoingia? Hiyo haitoshi, wakati wa Mkurugenzi (Mstaafu sasa) Dkt Paul Msemwa, ukifika pale unaona kabisa kwamba kuna linalofanyika. Lakini toka aondoke mambo yamekuwa mabovu sijapata kuona. Dkt Msemwa alisimamia Makumbusho ya Taifa ya Nyumba ya Sanaa pawe mahali pa kukutanika jamii na kuona ya kale na mapya pamoja na kupata buruduani. Akisaidiwa na Kamati ya Ushauri Dkt Msemwa alitembea nchi kadhaa duniani kuona jinsi ya kuboresha makumbuzho ya Taifa ili dhana ya kwamba ni mahali pa kuhifadhia kumbukumbu za kale tu itoweke na badala yake kial mtu aje pale na familia yake kuona hayo ya kale na ya sasa. Unaambiwa kuna ukumbi wa kuchukua watu 500 kwa wakati mmoja, uliza bei yake, utaambiwa kukodisha na kufanya shughuli zako pale ni shilingi milioni 1.5m/- Sasa jiulize vikundi vya utamaduni ambavyo havina mahali pa kuoneshea kazi zao vitamudu kweli bei hiyo? Haya, pana studio za kisasa za kurekodia muziki. Hadi leo umeosikia kuna kazi inafanyika pale? Rais Kikwete alipita mwaka juzi na kukuta maonesho ya soka na wanasoka wa Tananzaia, akaagiza kufanyike utaratibu wa kuwa na holi la kuwa na historia ya wanamichezo wote wa Tanzania (kina Kinyogoli, Filbert Bayi, Suleiman Nyambui, Gidamis Shahanga na kadhalika) pamoja na wanamuziki kina Mbaraka Mwinshehe, Salum Abdallah, na kadhalika pamoja na kina Mwinamila na wengineo) lakini hadi leo agizo hilo halijatekelezwa. Kwa ujumla Makumbushoa ya Taifa na Jengo la utamaduni ni kinyume na matarajio ya serikali. Wafanyakazi wazembe, usimamizi mbovu na hauna tina wala ubunifu, na juu ya yote ni taasisi iliyoshindwa! Tunaomba waziri ama wizara husika itupie jicho makumbusho ya Taifa kwani ni jicho la Tanzania ya leo na ya kesho. Ikiwezekana Dkt Paul Msemwa arejeshwe kwa muda wa miaka mitatu ama minne aweke mabo sawa. Hawa waliopo ni bure kabisa.

    ReplyDelete
  3. Kama serikali haitoi pesa za kuwawezesha wafanyaje jamani? Lakini hili la watoto kuanguka na mimi nimeliona tena muda mfupi baada ya kumuhoji mkurugenzi wa Makumbusho hiyo juu ya sherehe za wanawake. Nilimwona anazungumza tu na watu bila kushtuka.

    ReplyDelete
  4. Kwakweli mimi kama mzazi nimeumia sana, huu ni unyama na si ubinadamu, viongizi hao walipaswa kushtushwa na tukio hilo kwa kwakweli wazazi sasa tutaogopa kuwaruhusu watoto wetu waende makumbusho hiyo kama watu wenyewe hawajali watoto wetu. Unyama mkubwa huu. Imeniuma sana.

    ReplyDelete
  5. Mungu awasamehe hao viongozi kwakweli. Kwaresma hii Yes kesha wasamehe. Mungu bariki watoto wetu wanaoenda makumbusho.

    ReplyDelete
  6. Serikali nailaumu mimi. Iweinaendesha semina na ukaribu kwa wageni. Pia tulishautumia ukumbi wao wa mikutano unajoto kama handaki, mara ya kwanza tulipo kutana na kakijana kafupi kananywele nyingi kakatuambia kuwa utashughulikiwa mara ya pili kakasema hivyo hivyo we subiri kakirudia tena kutetea ujinga tutakachapa makofi.

    ReplyDelete
  7. Waziri Nyalandu linda Tembo baba acha makumbusho ijifie, kwani shingapi? au hujui yembo wakipotea historia yao itabaki makumbusho? Acha hizo mzazi.

    ReplyDelete
  8. Msisumbuke bure na makumbusho, iacheni kama ilivyo kwani ilishakosa dira muda mrefu sana, hata wizara inajua ndo mana haitaki kuunda Bodi, haitaki ajira zilizopitishwa, shirika linaendeshwa na jeshi la mtu mmoja lisilotaka wenye taaluma au wanaotoa ushauri wa kujenga. ukishauri tu unapigwa uhamisho wa maana hata kama ajira yako ilitokana na madhumuni maalum! shangaa!!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...