Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam limeanza kumhoji Askofu JOSEPHAT GWAJIMA wa Kanisa la Ufufuo na Uzima baada ya kujisalimisha kama alivyotakiwa kufanya hivyo na Kamishana wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam.

Askofu Gwajima alifika kituo kikuu cha Polisi saa nane na dakika kumi na tano mchana wa tarehe 27/03/2015. Mara baada ya kufika kituoni hapo alielekezwa kwenda kumuona Mkuu wa Upelelezi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam SACP Constantine Masawe ambaye alikuwa akisubiri kufika kwake.

Tuhuma zinazomkabili Askofu Gwajima ni pamoja na kumkashfu na kumtukana hadharani Kiongozi wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo.

Taratibu za mahojiano zimekwishaanza kwa mujibu wa sheria na mtuhumiwa atapewa haki zote anazostahili kama vile kuwa na ndugu yake wa karibu, rafiki yake anayemwamini au wakili wake. 

Kama ilivyo kawaida utakusanywa ushahidi kutoka pande zote za shauri hilo ili kubaini ukweli wa jinsi tukio hilo lilivyotokea na athari zake.

Baada ya hapo hatua nyingine za kisheria zitachukuliwa ikiwa ni pamoja na kupata maoni ya kitaalamu na ya kisheria ili kuhakikisha kwamba haki inatendeka. Ili ufanisi upatikane katika upelelezi wa shauri hili, ni muhimu kupata ushirikiano kutoka kwa kila atakayetakiwa kulisaidia Jeshi la Polisi kukamilisha haraka upelelezi wa shauri hili ambalo sasa limepata mvuto mkubwa katika jamii.

Imetolewa na:
S. H. KOVA
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Mtumishi wa mungu gwajima amrudie mungu wake hasa ktk kipindi hiki cha kwaresma kwani anayekosa ni binadamu.

    ReplyDelete
  2. Mtumishi wa mungu gwajima amrudie mungu wake hasa ktk kipindi hiki cha kwaresma kwani anayekosa ni binadamu.

    ReplyDelete
  3. Nimevutiwa na taarifa hii, maudhi yake yametolewa kistaarabu kabisa. Natamani taarifa zinazohusu watuhimiwa wote ingetolewa kwa namna hii na jeshi letu la polisi bila kujali ni nani anakabiliwa na tuhima husika.
    Amani Daima

    ReplyDelete
  4. Serikali pls kuweni makini na maamuzi ya ili jambo na tungependa msiwaachie Polisi pekee kufanya maamuzi yoyote yale na Wanasheria wa Serikali wenye uzoefu mkubwa muweze kuwasaidia Polisi.

    Mimi binafsi ni Mkristo tena Roman Catholic lakini hapa sifungamani mahali popote, Huyu bwana Gwajima ana wafuasi wake walio wengi sana na Mh Pengo ana wafuasi wake wengi sana ila ningemuomba Mh Rais na Wazee wengine wengi wa nchi hii wenye busara mfanye maamuzi yaliyo mazuri kwa nchi yetu ili hii issue isije ikaleta impact yoyote kwa wahusika, kwa wananchi na kwa taifa na ningependa Muwakutanishe hawa watu na waondoe tofauti zao maana itakuwa ni mara ya kwanza watu wa dini kutokwa na roho mtakatifu na kuamua kuchukua jaziba na kuhusisha Polisi badala ya kuwa kama Yesu aliyesema atakae kupiga shavu la kushoto basi mpatie shavu lingine na kusamehe. HAPA NIMESHANGAZWA KUONA HEKIMA YA BIBLIA NA MAANDIKO IMEWEKWA PEMBENI.

    Wazee wote wenye busara wa Kanisa na Maaskofu ndani ya nchi hii ninawaomba muingilie kati ili swala na ningewaomba muwaombe Polisi kusitisha maamuzi yao yoyote na Polisi mngewaomba hawa wazee wawasaidie ili kuondoa hii tofauti iliyopo kwa hawa watu wanaounganisha mamia ya waumini wao.

    Kwa Kuenzi misingi ya nchi hii kwa jinsi ilivyoundwa ningeshauri pia hii nchi ibaki kama ilivyokuwa mwanzo isifungamane ktk dini yoyote na isiwe na dini kabisa. Tusikubari ata siku moja Siasa za aina yoyote ikatufanya tuweke dini ktk nchi hii yetu nzuri tuliyorithi kwa Wazee wetu. Wewe mwanasiasa eidha wa dini yoyote Usikubari kutupeleka pabaya kwa kuwa wewe ni dini gani na kwakuwa leo una cheo au eidha unategemea nafasi gani kisiasa ktk uchaguzi baadae. Wazee wangu wote walio ndani ya Usalama wa Taifa ningependa na ningeomba mfanye analysis nzuri kuhusu ili swala na maswala hayo ya Mahakama ya kadhi na kuishauri Serikali kikamilifu na sio kwamba nawachukia ndugu zangu Waislam hapana kabisa tena Mke wangu ni Muislam na mmoja wa watoto wangu ameoa Muislam hivyo sina tatizo na hawa ndugu zangu bali nisingependa Taifa ili liwe na udini wowote ule ili watoto wetu wabaki kuwa na amani kama tuliyorithi sisi toka kwa Mababu zetu na tubaki kuoana na kusaidiana na kuwa wamoja! Nashangaa leo hii Taifa ili eti linataka kuwa na dini, linataka kuwa na mahakama za dini na linataka kuwa na makabila! hivi sisi ni akina nani haswa?! Kama wasingekuwa wakoloni wazungu na waarab kuja Afrika hivi sisi leo tungejua ukristo na uislam??! Basi nawaomba wenye maamuzi eidha Wabunge, Mawaziri, Mkuu wa nchi tunaomba ndani ya nchi yetu ibaki kuwa bila dini na daima Tanzania itabaki kuwa Taifa Kubwa na lenye Amani hapa duniani. Mkumbukeni Baba wa Taifa na Maono yake na tuelekeze nguvu kuifanya Tanzania kuwa taifa lenye nguvu Afrika na duniani badala ya kutafuta Mahakama za dini na kuendekeza ukabila.

    Nimechukua muda wangu na kutumia haki yangu ya demokrasia kuzungumzia yaliyomo moyoni mwangu kwa Manufaa ya Taifa ili na watoto wetu na Kizazi kijacho.

    Mungu ibari Tanzania, Mungu Ibariki Afrika na Mungu Wabariki Mh Pengo na Mh Gwajima ili warudi makanisani na sio kubaki Polisi na Mahakamani.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...