Balozi wa Tanzania nchini Malaysia Dkt. Aziz Ponary Mlima akiwasilisha Hati za Utambulisho kwa Sultani wa Brunei Mheshimiwa Haji Hassanal Bolkiah Mu'izzaddin Waddaulah Ibin Al-Marhum Sultan Haji Omar 'Ali Saifuddien Sa'adul Khairi Waddien ambaye ni Sultan na Mtawala wa Brunei Darussalam, Kwa ufupi hii ni moja ya nchi zenye watu wachache, utajiri mkubwa wa mafuta na kiwango kizuri cha maisha ya wananchi wake wenye kipato cha wastani cha USD 43,000 kwa mwaka. Pato la taifa na uchumi unategemea zaidi mafuta na gesi na sekta zingine.
 Balozi Dkt. Aziz Mlima pia alifanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje Mheshimiwa Paduka Seri Waziri Sahibul Himmah Mohamed Bolkiah na vile vile alionana na Waziri wa Nchi wa Mambo ya Nje II Dato Seri Awang Lim Jock Seng na atakuwa na mazungumzo na Waziri wa Elimu Dato Seri Haji Awang Abu Bakar bin Haji Apong.
 Dkt. Aziz Ponary Mlima pamoja na mabalozi kutoka Afghanstan, Korea Kaskazini Palestine, Iraq, Spain na Ghana katika picha ya pamoja leo hii  bada ya kuwawasilisha Hati zao za Utambulisho na kuwa rasmi mabalozi wasio wakazi kwa nchi ya Brunei Darussalam.
 Balozi Dkt. Aziz P. Mlima na Naibu Balozi Bwana Rogatius Shao (kulia)   baada ya kuwasilisha hati za utambulisho leo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...