Waziri  mpya wa Nishati na Madini,George Simbachawene (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati makabidhiano ya ofisi na Aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini,Profesa Sospeter Muhongo,leo jijini Dar es Salaam.
Waziri  mpya wa Nishati na Madini,George Simbachawene (kulia) akikabidhiwa rasmi nyaraka za ofisi na Aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini,Profesa Sospeter Muhongo,leo jijini Dar es Salaam.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii 

Aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini,Profesa Sospeter Muhongo amesema uadilifu unahitajika katika sekta ya Nishati na Madini pasiwepo na rushwa kwani hiyo ni kuweza kusaidia watanzania masikini wanaongalia sekta hiyo kwa maendeleo ya uchumi wao.

Muhongo ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akikakabidhi ofisi kwa Waziri  mpya wa Nishati na Madini,George Simbachawene,amesema lazima kuwepo na uzinagatiaji wa mikataba ili watanzania waweze kunufaika na rasilimali zao.

Muhongo amesema Simbachawene sio mtu wa tamaa siku zote alipokuwa Naibu wa Waziri wa Nishati na Madini walikuwa wakiambiana juu ya kuwatumikia watanzania wengi na sio mtu binafsi.

Amesema lazima tujenge uchumi imara kutokana na sekta hii ili watanzania waweze kukua kiuchumi kutokana na sekta ya madini inavyokua kwa kasi.

Muhongo amewataka waandishi kuelimisha watanzania kwa ajili ya ustawi wa taifa na sio mtu mmoja au ubinafis wa mtu.

Kwa upande wa Simbachawene amesema ataendeleza mazuri yaliyoachwa na mtangulizi wake kwa  kuweka uwazi kwa kila kitu kinachofanyika,kwani ofisi ya umma sio mali ya mtu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Tunamshukuru Mheshimiwa Rais kwa kututeulia mchapa kazi na mwadilifu baada ya majungu kumuondoa mwadilifua na mchapakazi mwingine aliyekuwa anaangalia maslahi ya taifa na watanzania maskini.

    Tunatarajia makubwa kutoka kwa Mheshimiwa Simbachawene.

    Kwa wazee wa majungu na visasi na tamaa mwacheni waziri achape kazi na atutumikie watanzania.

    ReplyDelete
  2. haya ndio matokeo ya siasa ya maji taka za watanzania. hatutaki watendaji tunataka watu wanaotudanya na siasa zoa. Muhongo is a guy of action. ndio maana hata EAC hawatutaki si watendaji sisi bra bra tuu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...