Na Mwandishi Wetu

MPAMBANO wa ngumi wa kufungua mwaka unatarajiwa kupigwa Ifakara mkoa wa Morogoro  kuhamasisha na kukuza mchezo wa masumbwi nchini. promota wa mpambano huo Hiari Bohari amesema kuwa kwa sasa anataka aendeleze mchezo wa masumbwi Ifakara kwa kuwa watu wapo na mchezo unapendwa.

Alisema siku hiyo ya January 2. 2015 itakuwa ni siku ya kufungua mwaka kwa mpambano wa masumbwi kati ya Abdallah Kilima na Abdul Amwenye huku Saleh Makuka akipambanma na Said Chamaki

Aliongezea pia  kutakuwa na mapambano mawili kwa ajili ya kuhamasisha wanawake waje washiriki katika michezi ya ngumi ambapo siku hiyo Aika Georger atapambana na Najma Ally.

Bohari ameomba  wadau mbalimbali kutoa sapoti na kumuunga mkono katika harakati za kuinua mchezo wa masumbwi ili uweze kusonga mbele.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...