Afisa
Habari wa kituo cha Sheria na Haki za Binadamu mkoani Kilimanjaro
(KWIECO), Veronica Ollomi akifafanua jambo katika Warsha ya siku mbili
kwa waandishi wa Habari wa mkoa wa Kilimanjaro, kilichofanyika
juzi mjini Moshi, kwa lengo la kuwapa mafunzo juu ya Haki za Binadamu
na Sheria zake.
Washiriki wa Warsha ya Haki za Binadamu, waandishi wa
Habari mkoani Kilimanjaro wakisikiliza kwa makini wakati wa
uwasilishaji wa mada mbalimbali katika mafunzo hayo, yakiwemo swala la
Wosia, Sheria ya Ardhi kwa Lengo la kuwawezesha kupata uelewa wa
sheria hizo katika utendaji wao wa kazi.
Mtangazaji wa Redio Moshi FM, Neema Mkotya akiweka
sawa mitambo kabla ya kuwasilisha Mada.
Mtaalamu wa maswala ya Haki za Binadamu kutoka
KWIECO, Elizabeth Mushi akifafanua jambo kwa washiriki wa Warsha
hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...