Mkurugenzi wa kwaya ya ‘Family Singers’ Daniel Misheto (kulia). 

WAZIRI MKUU, Mizengo Pinda ametajwa kuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa albamu ‘Usilie’ ambayo itapatikana kwenye DVD Desemba 7, mwaka huu.
Akizungumza Dar es Salaam jana kwenye mkutano na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa kwaya ya ‘Family Singers’ Daniel Misheto, alisema hafla hiyo itafanyika kwenye Ukumbi wa PTA uliopo Uwanja wa Sabasaba, Dar es Salaam.
Mbali ya uzinduzi huo Misheto alisema pia wasanii mbalimbali wa filamu watanogesha siku hiyo.
 Aliwataja waimbaji wa injili ambao watakuwepo siku hiyo kuwa ni Leah Mudy, AIC (T) Vijana Chang’ombe, Accasia Singers, Papson Mastaki kutoka Kenya na Frank Hume kutoka Boston nchini Marekani watatumbuiza.
Uzinduzi huu umeratibiwa na Misheto Promotion, ambapo kabla ya uzinduzi huo kutafanyika huduma za bila malipo za kiafya na kitabibu kutoka kwa madaktari bingwa wa magonjwa mbalimbali, ambayo yamekuwa yakiikabili jamii.
Misheto ameyataja magonjwa hayo kuwa ni moyo, figo, kisukari na mengineyo ambapo huduma hiyo itatolewa na madaktari bingwa nchini. Picha zote na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
“Huduma hii itaanza saa mbili asubuhi na itatolewa bure, ikiwemo ushauri na kwa wale ambao wataweza kutibika watatibiwa, ila ambao watakuwa kesi zao zimekuwa ni kubwa zaidi watapewa ushauri wa bure wa kuendelea na matibabu katika hospitali kubwa na hakutakuwa na kiingilio," alisema Misheto.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. albam ya "usilie" ila jamaa huwa analia.

    ReplyDelete
  2. Pinda bado atakuwepo tarehe hiyo?! Mmhh nchi nzuri sn hii wezi kuitwa malaika wanaosimamia wizi kuitwa miungu.

    ReplyDelete
  3. Utashangaaaa yaani we acha tu.....

    ReplyDelete
  4. Ndugu zanguni watoa maoni namba1 na 2 hapo juui, mngekuwa na mapenzi ya dhati na nchi yetu Tanzania, tungewaona katika mkutano wa wanadiaspora mwezi augusti 2014 Dar es salaam. Kwa wale tuliokuwepo tulipata nafasi ya kukutana na hata kufanya mazungumzo ya faragha na viongozi wetu wa juu wa serikali yetu. Mimi binafsi nilipata nafasi hiyo ya kuongea na Mhe. Waziri Mkuu Pinda faragha Serena Hoteli tarehe 16 agosti 2014. Ni mtu mwelewa na mwenye upeo wa hali ya juu ya kuelewa mambo na msikivu. Na ni mtu wa kawaida kabisa ukiwa ukiongea naye. Kumwita mwizi, mimi sitawaelewa inavyotakiwa niwaelewe na mueleweke ninyi juu yake. Msg delivered.

    Peters Mhoja - Sweden

    ReplyDelete
  5. Mr. Mhoja mtu anaweza kuwa mtu mzuri sana. Hapa hatuongelei uzuri wa mtu, tunaongelea uongozi na kusimamia yale majukumu uliyokabidhiwa. Mwalimu Nyerere aliwahi kusema "kama unachagua kiongozi kwa uzuri wa sura yake, nenda kanywe naye chai" Hapa tunaongelea uongozi na uwezo wa kusimamia majukumu yake aliyokabidhiwa. Nothing personal.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...