Mkurugenzi Mkuu wa TFDA , Bw. Hiiti B. Sillo akitoa hotuba ya TFDA
kukubali kujiunga na Umoja wa Nchi za Asia katika Udhibiti wa Vifaa Tiba na
Vitendanishi (Asian Harmonization Working Party on medical devices and
diagnostics - AHWP) wakati wa mkutano wa mwaka wa AHWP uliofanyika Seoul, Korea
Kusini kuanzia tarehe 17 - 21 Novemba 2014. Tanzania imekubaliwa rasmi kuwa mwanachama
24 wa AHWP ikiwa ni
nchi ya pili Barani Afrika
kujiunga na umoja huo baada ya Afrika Kusini.
Mkurugenzi Mkuu
wa TFDA, Bw. Hiiti B. Sillo akiwa na Mwenyekiti wa umoja huo Dkt. Saleh Al
–Tayyar kutoka Saudi Arabia baada ya kukabidhiwa
mwongozo rasmi TFDA wa kuimarisha mfumo wa udhibiti wa vifaa tiba na
vitendanishi kama mwanachama mpya wa umoja huo.
Mwenyekiti
wa AHWP , Dkt. Saleh Al –Tayyar
kutoka Saudi Arabia akiwapongeza Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Bw. Hiiti B.
Sillo na Meneja wa Udhibiti wa Vifaa Tiba, TFDA, Bi. Agnes Sitta Kijo, baada ya
Tanzania kujiunga rasmi kuwa mjumbe wa Umoja wa Wadhibiti wa Vifaa Tiba katika
nchi za Asia (AHWP).
Mkurugenzi Mkuu
wa TFDA, Bw. Hiiti B. Sillo akisalimiana na Waziri
anayesimamia Usalama wa Chakula na Dawa nchini Korea na kati yao ni
Mwenyekiti wa AHWP Dkt. Saleh Al –Tayyar
.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...