Wiki hii, Ubalozi ukiongozwa na Mama Balozi Rose Mero umeshiriki kwenye maonyesho ya UN ya kina mama, Geneva (United Nations Women's Guild 2014), yenye lengo la kukusanya pesa za kusaidia miradi ya kuendeleza watoto wenye mahitaji mbalimbali duniani kote.

Kwenye maonyesho hayo, banda la Tanzania lilijumuisha bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na kutengenezwa nchini Tanzania ikiwa ni pamoja na kahawa, majani ya chai, khanga, vitenge, vinyago, korosho n.k

Watu mbalimbali walipata nafasi ya kujipatia chakula cha kitanzania kama vile maandazi, chapatti, samaki wa kukaanga, maharage ya kuungwa na Nazi, chai yenye viungo vya tangawizi, sambusa, pilau, n.k
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, alipata nafasi ya kutembelea banda la Tanzania akiwa Geneva kuhudhulia kikao cha Bodi ya " Water Supply and Sanitation Collaborative Council", ofisi zake Geneva, kwa nafasi yake kama Mwenyekiti.Kulia ni Balozi wa Tanzania katika Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Geneva, Mhe. Modest Mero

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...