Dar es Salaam. Mbunifu wa mitindo na
muigizaji wa filamu nchini, mrembo Jokate Mwegelo kwa kushirikiana na mshiriki
maarufu wa Big Brother Africa, Mganda Gaetano Kagwa wameteuliwa kuendesha
kipindi kipya cha Maisha kijulikanacho kwa jina la “Beat the Challenge” kupitia
M-Net East Africa.
Kipindi kitashindanisha familia
mbalimbali katika nchi za Tanzania, Kenya na Uganda na mshindi atapewa gari
jipya kabisa kutoka kwa waandaaji.
Katika mashindano hayo, kila
familia inatakiwa kuwa na watu wanne ambao ni Baba, Mama na watoto wawili
wenye umri kati ya miaka 12 na 17.Familia hizo zitashinda katika
kutatua changamoto mbalimbali zitakazowasilishwa na waandaaji na kila familia
itakuwa na jukumu la kutatua hiz changamoto kwaa kutumia nguvu kuliko ufahamu
wa akili.
Akizungumza jana, Jokate alisema
kuwa amejisikia faraja kubwa kupewa nafasi hiyo ambayo itampa uzoefu zaidi
katika fani ya utangazaji na kujipanua kimawazo.Jokate ambaye pia ni Miss Tanzania
namba mbili wa mwaka 2006 alisema kuwa anajisikia faraja kubwa kwa kuzidi
kuongeza wigo wa mawasiliano kwani hii si mara yake ya kwanza kuendesha vipindi
katika televisheni baada ya kutamba katika kipindi cha Chaneli O.
“Kama nilivyosema, nataka kuishi kwa
kutegemea vipaji vyangu na wala si vinginevyo, nimeanza katika urembo, nikaja
katika ubinifu na uanaminitindo, MC, muigizaji wa filamu na sasa mtangazaji,
kote huko nimefanikiwa, ni faraja kubwa kwangu,” alisema Jokate.
Alisema kuwa anashukuru kuona kuwa
filamu yake ya Mikono Salama kwa sasa inatamba sana na inamuongezea sifa kubwa
katika fani hiyo. “Hata kidoti Fashion nayo inatamba, hivyo kwa nashukuru Mungu
kwa kuniwezesha,” alisema.
Kwa upande wa Tanzania, utafutaji wa
washiriki utafanyika Jumamosi Novemba 22), New Africa Hotel, wakati Uganda
watafanyia kwenye hotel ya Silver Springs, Kampala na Kenya kwenye studio za
Supersport zilizopo katika Barabara ya Jamhuri.Kipindi cha kwanza kitarushwa
Desemba 13 kupitia chaneli ya Maisha Magic 161 kuanzia saa 2.30 usiku kwa
mujibu wa Jokate.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...