Na John Kitime
LEO tunatimiza miaka kumi toka kifo cha mwanamuziki mahiri Freddy Supreme au maarufu kama Ndala Kasheba. Freddy alianza kufundishwa gitaa na baba yake wakati akiwa na umri wa miaka 12. Baba yake alijua kupiga gitaa japo hakufanya kazi ya uanamuziki, alikuwa akipiga gitaa nyumbani baada ya saa za kazi.
Moja ya bendi maarufu ambazo zilimtambulisha sana Fredd ilikuwa Orchestra Fauvette, Freddy alieleza kuwa bendi ya Orchestra Fauvette ilianza tarehe 7 mwezi wa sita mwaka 1964 katika jiji la Lubumbashi huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.
Jina hilo Fauvette kwa kiswahili ni Chiriku, bendi ilikuwa na muimbaji ambaye waliamini alikuwa anaimba kama chiriku na hivyo kuipa bendi hiyo jina hilo.
Vyombo vyao vya muziki walinunua Ujerumani kupitia duka la muziki la Dar es salaam Music House (duka lipo mpaka leo). Vyombo vilikuwa vya aina ya Hofner, jina lililoheshimika sana kwa wanamuziki wakati huo. KUSOMA HABARI KAMILI BOFYA HAPA
Freddy "Supreme" Ndala Kasheba akitumbuiza umati wa washabiki katika bustani ya Mnazi Mmoja mwaka 1980
Freddy "Supreme" Ndala Kasheba akitumbuiza mabalozi wakati walipofanya semina elekezi katika hoteli ya kitalii ya Ngorongoro Februari 2007
Ankal akisikiliza wimbo wa "Yellow Card" wakati Kasheba alipokuwa akimalizia kuurekodi katika studio za Makuti zilizokuwa Shariff Shamba jijini Dar es salaam mwaka 2006. Usikilie hapa chini
Freddy "Supreme" Ndala Kasheba akisalimiana na Balozi Mohamed Maharage wakati wa semina elekezi kwa mabalozi katika hoteli ya kitalii ya Ngorongoro Februari 2007.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Michuzi unazingua sasa, kama picha ni za February 2007, mbona miaka kumi haijafika? Hebu weka mambo sawa.

    ReplyDelete
  2. Michuzi nakubaliana na wewe, enzi hizo pembeni kuna kidongo chekundu unakwenda sikukuu kama ya idd kusherekea baada ya kupatiwa visheti, na mapochopocho mengine. Utaratibu huu haupo siku hizi!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...