Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (kushoto) akizionesha kadi za Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) baada ya kukabidhiwa na Katibu wa Kata ya Lionja, Wilayani Nachingwea, Hashimu Halifa (kulia). Waliorudisha kadi hizo na kujiunga na CCM ni Lusia Mohammed, Abdu Ngawina na Mohammed Kindamba. Waziri Chikawe ambaye yupo katika ziara ya kikazi jimboni kwake aliwaomba Wajumbe wa Mabaraza ya Jumuiya zote za CCM Kata, Viongozi wa Dini na Wajumbe wa Baraza la Wazee katika Kata hiyo kuhakikisha chama kinaimarishwa zaidi na kuwakaribisha wanachama wote wanaotoka vyama vingine ili wajiunge na CCM.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe akizungumza na Wajumbe wa Mabaraza ya Jumuiya zote za CCM Kata ya Lionja, Viongozi wa Dini na Wajumbe wa Baraza la Wazee katika Kata hiyo, Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi. Waziri Chikawe ambaye yupo katika ziara ya kikazi katika Jimbo lake la Nachingwea aliwaomba wajumbe hao kuhakikisha chama kinaimarishwa zaidi na kuwakaribisha wanachama wote wanaotoka vyama vingine ili wajiunge na CCM.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (kulia) akizungumza na Mjumbe wa CCM Kata ya Lionja ambaye ni mlemavu wa miguu, Hassan Chingwale baada ya kumaliza kikao chake na Wajumbe wa Mabaraza ya Jumuiya zote za CCM Kata, Viongozi wa Dini na Wajumbe wa Baraza la Wazee katika Kata hiyo, Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi. Waziri Chikawe yupo katika ziara ya kikazi jimboni mwake, aliwaomba wajumbe hao kuhakikisha chama kinaimarishwa zaidi na kuwakaribisha wanachama wote wanaotoka vyama vingine ili wajiunge na CCM. Picha na zote na Felix Mwagara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Ni njaa zao tu hapo hakuna mwenye mapenzi ya kweli.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...