Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha pamoja na Wadau wa Sekta ya Utalii nchini wanayofuraha ya kuwakaribisha Wananchi wote na Wadau mbalimbali katika Maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani kwa mwaka 2014 ambayo Kitaifa yatafanyika Mkoani Arusha kwenye viwanja vya Nane Nane (TASO) kuanzia tarehe 20 hadi 28 Septemba, 2014.

Siku ya Utalii Duniani huadhimishwa tarehe 27 Septemba ya kila mwaka ambapo kila nchi mwanachama wa Shirika la Utalii Duniani (UNWTO) husherekea siku hii, kwa lengo la kuweka uelewa kwa Jamii kuhusu umuhimu wa utalii na thamani yake, kijamii, kisiasa, kitamaduni na kiuchumi.

Kauli Mbiu ya Mwaka huu ni “Utalii na Maendeleo ya Jamii’’ (Tourism and Community Development) kwa kuzingatia Kauli Mbiu hii, tunawajulisha wadau wote katika nyanja mbalimbali za Utalii, Maliasili na Uhifadhi, vikundi vya jamii na wajasiriamali, viongozi na wataalamu kwa pamoja kushiriki kikamilifu katika Maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani kwa nia ya kujifunza na kutambua fursa za kiuchumi zilizopo katika Sekta ya Utalii na kutumia fursa hizo kujikomboa katika umaskini.

Shughuli zitakazofanyika ni pamoja na kuwasilisha na kuonesha na kwa vitendo juu ya tafsiri ya Kauli Mbiu kwa kufanya kongamano la ushirikishwaji wa jamii kwenye sekta ya Utalii kwa ajili ya kujiletea maendeleo, mashindano ya Uchoraji wa picha kuhusiana na kauli mbiu, michezo na burudani mbalimbali.

Vilevile kutakuwa na maonesho ya utalii, malikale, misitu na masuala ya uhifadhi kwa ujumla na bila kusahau ziara ya kutembelea Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na Hifadhi ya Taifa ya Arusha kwa nia ya kuhamasisha wananchi kushiriki kwenye shughuli za utalii wa ndani.

Wito unatolewa kwa kuwaalika wadau wote wa utalii na jamii husika kuja kwa pamoja na kuadhimisha siku hii kama ishara ya jitihada za pamoja za kufanya utalii nguzo ya kweli ya maendeleo ya Jamii nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...