Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Doris Malulu akipeana mkono na Mwenyekiti wa Kijiji cha Kambi ya Simba, Damian John wakati wa makabidhiano ya mfano wa hundi ya Sh. Milioni 45 zilizotolewa kwa ajili ya kuchimba kisima cha maji kijijini hapo mwishoni mwa wiki. Wengine ni Meneja Mauzo TBL Mkoa wa Arusha Richard Temba (mwenye miwani) na Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Karatu Moses Mabula.
 Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Doris Malulu akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kambi ya Simba, Kata ya Mbulumbulu wilayani Karatu, Arusha, wakati wa hafla ya kuwakabidhi mfano wa hundi ya sh. mil. 45 za kugharamia uchimbaji wa kisima cha maji kijijini hapo, mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Meneja Mauzo TBL Mkoa wa Arusha Richard Temba na aliyekaa ni Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Karatu, Moses Mabula.
 Wananchi wa kijiji hicho wakishuhudia makabidhiano ya hundi hiyo
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya wilaya ya Karatu, mkoani Arusha, Moses Mabula na Meneja Mauzo TBL Mkoa wa Arusha Richard Temba wakiwa katika picha ya pamoja na Kamati ya Maji ya Kijiji cha Kambi ya Simba pamoja na watalaamu watakaochimba kisima hicho cha maji, baada ya kukabidhiwa mfano wa hundi ya Sh. Milioni 45 na TBL.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...