Na Rose Masaka - MAELEZO
WANANCHI mkoani Lindi wanatarajiwa kuelimishwa njia bora na za kisasa za
uvuvi, ufugaji na ukulima ili waweze kuboresha kipato chao na Taifa kwa ujumla.
Kauli hiyo imetolewa leo mjini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Jumuiya ya
Wakulima Tanzania(TASO) Engelbert Moyo wakati akiongea na waandishi wa
habari.
Amesema kuwa wakati wa maonesho ya nanenane ambayo Kitaifa yanafanyika
mkoani Lindi watajitahidi kuhakikisha wananchi wanajifunza teknolojia mpya
za kilimo, ufugaji na uvuvi ili waweze kuzalisha mazao yanayokidhi viwango vya
Kitaifa na Kimataifa.
Moyo ameongeza kuwa watawaelimu wavuvi juu ya madhara ya uvuvi haramu
na unavyohatarisha mazingira na viumbe wa majini.
Aidha Mwenyekiti huyo amesema kuwa maonesho yatafunguliwa na Rais wa
Serikali za Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt.
Ali Mohamed Shein na kufungwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
Amesema kuwa Mawaziri mbalimbali watasaidia kutoa elimu kwa wakazi
wa Mkoa huo kuhusu shughuli mbalimbali wanazozifanya katika kuwaletea
maendeleo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...